

*BANGI
Bangi ni aina ya dawa ya kulevya inayotokana na mmea
unaoitwa “Cannabis sativa” ambao hustawi na hutumika kwa wingi hapa
nchini na duniani kote. Bangi huathiri ubongo na kubadili jinsi tunavyotafsiri
uhalisia wa vitu. Majani na maua ya mmea huo hukaushwa na hutumiwa kama kilevi
peke yake au kwa kuchanganywa na dawa zingine. Mara nyingi bangi imekuwa ni
kati ya dawa ya awali kutumiwa, ambapo watumiaji wengi huanza matumizi wakiwa
na umri mdogo hivyo kuwa katika hatari zaidi kiafya, kijamii na kiuchumi.
Aidha, watumiaji wengi wa bangi huishia kutumia dawa nyingine hapo baadae kama
heroin na cocaine. Hivyo, bangi hutumika kama njia ya kuingia katika matumizi
ya dawa nyingine za kulevya. Majina mengine ya bangi yanayotumika mitaani ni
kama msuba, dope, nyasi, majani, mche, kitu, blanti, mboga, sigara kubwa,
ndumu, msokoto, ganja, nk.
MADHARA YA BANGI
Bangi iliyokaushwa, mbegu na misokoto
Matumizi ya bangi huchochea matumizi ya dawa nyingine za kulevya kwa namna mbili; kwanza kwa kuchanganya bangi na dawa nyingine za kulevya au kwa kuhamia kwenye dawa zingine kama heroin na cocaine. Hali hii huongeza madhara kwa mtumiaji na hata wakati mwingine husababisha vifo.
Kilimo haramu cha bangi mara nyingi hufanyika kwenye vyanzo vya maji, misituni na milimani ambapo miti hukatwa au kuchomwa moto na kusababisha kutoweka kwa baadhi ya viumbe hai na uoto wa asili, kukauka kwa vyanzo vya maji, mmomonyoko wa udongo na hatimaye ukame. Uharibifu huu umejidhihirisha katika safu za milima ya Uluguru, Usambara, Udzungwa na maeneo ya Arumeru.
Kushamiri kwa kilimo haramu cha bangi, kunaweza kusababisha uhaba wa mazao ya chakula na hivyo kupelekea kupanda bei ya vyakula na hata janga la njaa.
Kutokana na athari za matumizi na kilimo haramu cha bangi, Taifa linaingia gharama kubwa katika kukabiliana na tatizo hili, ikiwemo utoaji wa elimu mashuleni na katika jamii, matibabu ya maradhi mbalimbali, uteketezaji mashamba na udhibiti wa biashara haramu ya bangi.
Bangi huchangia kuongezeka kwa umasikini kwa mtumiaji, jamii na taifa kwa ujumla na kupelekea kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Utamsaidiaje mtumiaji wa bangi?
Mtumiaji anaweza kupunguza kiasi anachotumia taratibu na hatimaye kuacha.Aidha, asasi za kiraia huwasaidia watumiaji kuacha kwa kuwapa unasihi. Nyumba za upataji nafuu ‘sober house’ ambako hupitishwa kwenye hatua 12 za upataji nafuu. Kwa msaada zaidi tembelea tovuti www.zdcea.go.tz
Ujumbe kwa jamii
1. Wazazi, walezi na jamii kwa ujumla tuwalee watoto na vijana wetu katika maadili mema kwa kuwasikiliza, kuongea nao na kufuatilia maendeleo yao mara kwa mara.
2. Vijana wanashauriwa kujifunza na kuzingatia stadi za maisha ikiwemo kujiepusha na kukabiliana na makundi hatarishi yanayoweza kuwaingiza kwenye matumizi ya bangi.
3. Waathirika wa matumizi ya bangi wasinyanyapaliwe badala yake wasaidiwe na waelekezwe kwenye huduma stahiki
4. Bangi HAIONGEZI ufanisi na tija kazini, kwenye kilimo au masomo. Angalia jibu la swali hili hapa chini:-