*KHAT
Mirungi ni aina ya dawa ya kulevya
inayotokana na mmea unaoitwa โCatha edulisโ. Mmea huo una kemikali za
cathinone na cathine ambazo huongeza kasi ya utendaji wa mfumo wa fahamu.
Mirungi ilikuwa inatumika tangu enzi za mababu kwenye nchi za pembe ya Afrika
hususani Ethiopia, Eritrea, Kenya, Somalia pamoja na Rasi ya Arabuni nchini
Yemen.
Mirungi hutumika zaidi kwenye mikusanyiko ambayo hujumuisha zaidi wanaume
ingawa katika miaka ya karibuni wanawake wamejiingiza katika matumizi. Nchini kwetu
mirungi hustawi na hupatikana kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro- Same,
Tanga- Lushoto na Arusha Mlima Meru. Kiasi kingi cha mirungi huingizwa nchini
isivyo halali kutoka nchi jirani ya Kenya ambako ni zao halali la biashara.
Mirungi hufahamika kwa majina ya gomba, veve, miraa, kangeta, mkokaa, colombo,
asili, mbaga, alenle, nk.

MADHARA YA MIRUNGI
- Huongeza
kasi ya mapigo ya moyo hivyo kuweza kuongeza shinikizo la damu, kiharusi
na hata kusababisha kifo.
- Husababisha
vidonda vya utumbo mdogo, saratani ya mdomo, koo na tumbo
- Husababisha
upungufu wa msukumo wa kufanya tendo la ndoa, kumaliza haraka na kutoweza
kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu
- Hupunguza
ubora wa mbegu za kiume na kuvuruga mfumo wa utokaji wake na hata
kusababisha ugumba
- Mtumiaji
hukosa usingizi na ulevi ukiisha mwilini husababisha usingizi mzito
unaoweza kusababisha ajali hasa kwa madereva
- Huchochea
ukatili, fujo, ugomvi, kuongea sana masuala ya kusadikika na kuhangaika.
- Mtumiaji
hukosa kabisa hamu ya kula na kupungua uzito.
- Mirungi
husababisha upungufu wa maji mwilini na kuleta tatizo la kukosa choo
pamoja na ugonjwa wa bawasiri
- Mtumiaji
mirungi akiikosa mirungi hupata uchovu, sonona, hasira za ghafla,
kutetemeka, kushindwa kutulia na njozi za kutisha (night mares)
- Utumiaji
mirungi huozesha meno na yale yanayosalia hubadilika rangi, fizi kuuma na
harufu ya mdomo.
- Mirungi
huharibu ufanisi wa ini mwilini katika kuchuja sumu za mwili
- Mirungi
huamsha magonjwa ya akili yanayojitokeza kwa vipindi โmwezi mchangaโ kwa
watumiaji wenye tatizo hilo
- Wanawake
wanaotumia mirungi kipindi cha ujauzito wana hatari ya kupata maumivu ya
kifua, kuongezeka kwa mapigo ya moyo na msukumo wa damu
- Matumizi
ya mirungi yanaweza kusababisha kuzaliwa kwa watoto wenye uzito mdogo
ambao huweza kukataa kunyonya kutokana na ladha ya maziwa kubadilishwa na
viuatilifu vinavyotumika kwenye kilimo cha mirungi
- Watumiaji
mirungi hujikuta wakipenda kuvuta sigara au kunywa pombe wanapokosa
usingizi hivyo kudhuru zaidi afya zao.
- Mtumiaji
wa mirungi hutumia fedha ambazo zingekidhi mahitaji ya familia kununulia
mirungi hivyo kusababisha migogoro
- Utafunaji
mirungi hutumia muda mwingi na hufanyika muda wa kazi au muda ambao
mtumiaji hutakiwa kujumuika na familia yake hivyo kushusha uzalishaji na
ukaribu wa familia.
Sheria inasemaje kuhusu mirungi?
Mirungi katika taifa letu ni haramu.
Kujihusisha kwa namna yoyote na mirungi
(kulima, kuuza, kuhifadhi, kutumia, nk)ni KOSA LA JINAI na adhabu yake inafikia
hadi kifungo cha maisha
Baadhi ya nchi za Ulaya ambazo awali
ziliruhusu matumizi ya mirungi zimeanza kuiharamisha baada ya kuona madhara
yake
Utamsaidiaje mtumiaji wa mirungi?
Mtumiaji anaweza kupunguza kiasi
anachotumia taratibu na hatimaye kuacha.Aidha, asasi za kiraia huwasaidia
watumiaji kuacha kwa kuwapa unasihi. Nyumba za upataji nafuu โsober houseโ
ambako hupitishwa kwenye hatua 12 za upataji nafuu. Kwa msaada zaidi tembelea
tovuti www.zdcea.go.tz
Ujumbe kwa jamii
- Mirungi
HAIONGEZI ufanisi kazini, ufaulu katika masomo, udereva wala nguvu za
kiume.
- Wazazi
na walezi wawalee watoto katika maadili mema ikiwemo kuwa nao karibu na
kuwasikiliza.
- Vijana
wajifunze na kuzingatia stadi za maisha.
- Epuka
kutumia dawa za kulevya pamoja na kujiepusha na makundi hatarishi
yanayoweza kukuingiza kwenye utumiaji.